Sunday, May 15, 2016

UN Yaipongeza Tanzania kwa Uharaka wa Kuchunguza Tuhuma za Udhalilishaji wa Kijinsia.


Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mkutano  wa kupokea taarifa  kuhusu  jitihada zinazofanywa na Umoja wa Mataifa za kukabiliana na  tuhuma za  udhalilishaji wa kijinsia katika misheni za kulinda amani. Katika  mchango wake Balozi amesema Tanzania  haitawavumilia walinzi wa amani  wachache ambao wanaharibu kazi nzuri na sifa ya  kutukuka ya  JWTZ katika Misheni za Kulinda Amani za Umoja wa Mataifa. Na kwamba wale watakaothibitishwa kujihusisha na  tuhuma hizo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.
Naibu  Katibu Mkuu Mwandamizi, Bw. Atul Khare akitoa taarifa kuhusu mwelekeo na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na  vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia. katika taarifa yake ameipongeza  Tanzania  kwa namna ambayo iliitikia kwa haraka wito wa kuunda timu ya kitaifa ya uchunguzi ndani ya  siku tano  badala ya siku kumi kama taratibu zinavyoainisha na kwamba hatua hiyo ya  Tanzania  inapashwa kuigwa na  nchi nyingine
Na Mwandishi Maalum

Umoja wa Mataifa umeipongeza Tanzania kwa namna ambavyo imechukua hatua za haraka za kukabiliana na tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia zinazowahusisha baadhi ya walinzi wa amani wanaohudumu katika Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo( DRC)“Tanzania imeweza ndani ya siku tano tangu kupokea tuhuma dhidi ya walinzi wake wa amani kuunda timu ya kitaifa ya uchunguzi kwa ajili ya kuzifanyia kazi tuhuma hizo.

Hatua hii na utashi ulioonyeshwa na Tanzania ni hatua nzuri na inayopasha kupongezwa na inaonyesha namna gani inavyochukulia kwa uzito wa hali ya juu tuhuma hizo”.

Pongezi hizo zimetolewa mwishoni wa wiki ( Ijumaa) na Bw. AtulKhare, Naibu Katibu Mkuu Mwandamizi anayeongoza Idara ya Field Support katika Umoja wa Mataifa.

Mwishoni mwa wiki ,Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, aliandaa mkutano ambao ulikuwa na lengo la kutoa taarifa ya maendeleo na mwelekeo wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia zinazowakabili walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa, walinzi wa Amani wa Kimataifa, nawafanyakazi raia.

Katika taarifa yake, Bw. Khare amesema, utaratibu uliopo unaitaka nchi ambayo walinzi wake wametuhumiwa kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji pamoja na hatua nyingine, kuunda timu yake ya kitaifa ya uchunguzi ndani ya siku kumi, lakini  Tanzania iliunda timu hiyo ndani ya siku tano na kuanza kazi jambo ambalo amesisitiza linapashwa kuugwa na nchi nyingine.

Akabainisha kwamba kinachosubiriwa sasa kutoka Tanzania ni taarifa rasmi ya kukamilishwa kwa uchunguzi huo na hatua ambazo zitakuwa zimechukuliwa kwa walinzi ambao watakuwa wamethibitika kujihusisha na vitendo hivyo.

Tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya baadhi ya walinzi hao 
wa Amani wa Tanzania  ziliibuliwa na Umoja wa Mataifa mwezi March mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, amesema utovu wa nidhamu uliofanywa na walinzi wa chache hauwezi kuchafua kazi nzuri na sifa ya kutukuka ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Misheni mbalimbali za kulinda Amani chini ya Umoja wa Mataifa.

Akasema Balozi, ni kwa kutambua kazi hiyo ya kutukuka na ambayo pia imepelekea baadhi ya wanajeshi wa Tanzania kupoteza maisha yao kishujaa wakati wakiwasaidia wananchi wa mataifa mengine kuwa na amani. 

Tanzania inalichukulia kwa uzito wa kipekee tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia na kwamba wale wote wataokabainika hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akaongeza kwamba Tanzania imeamua kuwa ili wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa kwenda nchini Tanzania  ambapo watashirikiana na wakufunzi wa JWTZ katika kuimarisha mitaala ya ufundishaji inayohusiana na masuala ya ulinzi wa raia hususani eneo la udhalilishaji wa kijinsia.

Vilevile Balozi Manongi amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha kwamba vitendo hivyo viovu dhidi ya raia wasio kuwa na hatia vinakomeshwa ili pamoja na  mambo mengine kurejesha heshima ya Umoja wa Mataifa na heshima ya nchi zinazochangia wanajeshi na polisi katika misheni za kulinda Amani. 

Lakini kubwa zaidi kurejesha imani kwa wananchi wanaohitaji ulinzi.

Akielezea kwa ujumla kuhusu kadhia hiyo ya udhalilishaji wa kijinsi, Bw. Khare amesema, nchi nyingine zinazochangia walinzi wa Amani na ambazo pia walinzi wao wametuhumiwa zinaendelea ushirikiano kwa kuchukua hatua mbalimbali ingawa pia zipo zinazosuasua.
Nchi ambazo zimetoa ushirikiano ukiacha Tanzania ni Afrika ya Kusini,DRC, Misri na Bangladesh.

Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuwafikisha katika mahakama zakijeshi wale wanaokutwa na hatia, kufungwa, kufukuzwa kazi na kutoshiriki kabisa katika misheni za kulinda Amani na kutoa misaada kwa wahanga.

Akaongeza pia kwamba nchi nyingi zimeimarisha mitaala ya ufundishaji kwa walinzi wa amani, kuandaatimuzauchunguziambazozinakuwatayariwakatiwowotezitak

apohitajika, 

hukunyinginezikihakikishakwambazinakuwanawataalamuwamasual

ayasheriamiongonimwawalinziwa Amani.

Bw. 

KhareamesisitizaUmojawaMataifaunatambuamchangomkubwawaw

alinziwa Amani 

pamojanamazingiramagumuyautekelezajiwamamlakayao. 

Hatahivyoanasemavitendovyaudhalilishajiwakijinsiahavipashwikuvu

miliwawalakufumbiwa  macho 

nakwambakilanchiinaowajibuwakuwafikishambeleyamkonowasheri

awatuhumiwawanaothibitikakuhusikanaukatilihuonakwambaushirik

ianonamisaadakwawaathirikanijambo la muhimusana.


No comments: