SHIDA`S STORY OF HER LIFE AND THE DEATH OF HER PARENTs
NA.
MOHAMED HEMED
(Bizoman.com) +255(0) 655 450 234
Wazazi wake Shida walifariki miaka miwili
iliyopita, inavyosemekana walifariki katika hali ya utatanishi, ama kiukweli
tunaweza kusema wamepotea katika mazingira hatarishi ambayo ni hali ya kimiujiza
ama kiuchawi. Na kwa kweli haikujulikana imetokea kinamna gani, ila watu wengi
waliweza kulishutumu jambo hili kama ni masuala ya kiushirikina na uchawi
kutoka nyumbani kwao, sasa kwa hiyo hakuna mtu aliyekuwa na mashaka yoyote
katika hali hii. Shida Kwa sasa ni yatima. Baada ya kifo cha wazazi wake. Shida
aliamua kwenda kukaa kwa mjomba wake, Mr. Jongo ambaye anaishi na mke wake mama
Anna. Shida alikuwa mnyonge sana baada ya kuwapoteza wazazi wake vile vile
hakuwa na jinsi aliamua tu kwenda kuishi na mjomba wake Mr. Jongo. Mr. Jongo ni
mlevi na mtu msumbufu sana kwa wenzake. Anakunywa chupa tano (5) za gongo kwa
siku. Wakati anapolewa anakuwa anarudi nyumbani kwake usiku mkubwa sana na anakawaida
ya kumpiga mke wake pamoja na tabia yake mbaya aliyokuwanayo ya kwenda jikoni
kula nyama, chakula pamoja na vitu vyote vilivyoko huko jikoni, anakawaida ya
kuwaamsha watoto wake usiku wa manane na kuanza kuwapiga viboko, huku akisema
maneno ya kujinadi “Mimi ndo Jongo mtoto wa mzee Nyungunyungu, Amkeni nyinyi
wapumbavu! Nitawafundisha somo baya usiku huu.” Akiendelea kuwapiga na kuimba.
Kiukweli hiyo ndio iliyokuwa tabia yake ya kila siku kwani hakuijali sana
familiya yake wala mtu yoyote hususa katika nyumba yake. Shida alikaa kwa muda
mrefu sana ila alishindwa kustahamili na alitamani kuwa mbali na familiya hii
ila hakuwa na budi wala sehemu nyengine ya kwenda. Siku moja baada ya Shida
kuona mambo yanaweza kumshinda kuendelea kuishi katika nyuma hii alifikiri na
kuwaza na ndipo alipoamuwa kutoroka na kwenda kuishi kwa Shoga yake ambaye
anaishi nje kidogo ya kijiji alichokua akiishi yeye. Kijiji ambacho amekimbilia kina historiya mbali mbali
hususa katika masuala ya kiuchawi, Shida alishtuka sana baada ya kusikia ya kwamba
kijiji hichi kuna musuala ya kiuchawi, lakini hata hivyo ndani ya kijiji hichi
kinajali na kulinda sana utamaduni wao na kujiendeleza katika hali ya kiutamaduni,
kiuchumi na kimila. Pamoja na yote hayo na baadhi yake yalimchanganya kichwa
chake pale ilipofikiri na kuwaza nini haswa kikubwa kilichomleta katika kijiji
hichi kilicho na masuala ya ushirikina na hali ya kuwa wazazi wake binafsi
walifariki katika hali ya kiuchawi na hadi sasa hajui ni wapi ambako anaweza
kuonana na wazazi wake na leo hii anapata kusikia tena kuhusu uchawi, Shida
alichanganyikiwa sana hali ya kuwa ni mnyonge sana ila Shoga yake, aliamua kumtoa
wasi wasi kwa kutumia maneno matamu yamtoayo nyoka pangoni na miongoni mwa maneno hayo ni kama vile
yafuatavyo alisema hivi “Shoga yangu unajua
hapa kijijini petu kuna beach nzuri ambazo tunaweza kwenda kuzitembelea na
kupoteza mawazo? vile vile pana mbuga mbali mbali za wanyama hapa kijijini”.
Maelezo yote haya yalikuwa yakiendelea baina na Shida na Shoga yake baada ya
kupokelewa na wenyeji wake huko Buwalo Mkoani
Mwaza. Mama Anna na yeye huku
alihangaika kumtafuta Shida pale baada ya kukimbia na kuelekea kule ambako
kusikojilikana, Mama Anna alitumia jitihada ya hali ya juu kumtafuta mtoto wake
Shida ila hakufanikiwa kukutana nae na ndipo alipoamua kujipumzika nyumbani
kwake.
Ilipofika asubuhi ya siku ya pili mama
Anna na mume wake Mr. Jongo ambaye ni Mjomba wa Shida waliamua kuripoti katika
kituo cha polisi kilichopo karibu nao kwa ajili ya kupatiwa msaada na
mashirikiano kutoka kwa jeshi la polisi, hata hivyo jitihada zao zote zilishindikana
kumuona Shida kwani alikuwa mbali sana na kijiji hicho. Tukielekea kwa upande
wa Shida huko Buwalo mkoani Mwaza tayari mambo yake yameshaanza kuwa mazuri
baada ya wazazi wa Shoga yake kuanza kumsaidia na kumuwezesha katika masuala ya
kielimu. Shida alifikiriwa kusomeshwa kwanza na haikuchukua muda mrefu kuanzishwa
kusoma. Shida alionekana kuwa na fuhara iliyotokana na kuanza kwa masomo pamoja
na shoga yake. Kutokana na ufahamu mzuri aliokuwa nao Shida Walimu wake
walimpenda sana na vile vile walimpa kipaombele katika elimu na huku
wakimsisitiza sana hususa katika kutafuta elimu hata kama umbali wa kiasi gani,
hata hivyo pamoja na yote hayo Shida alipata
cheo cha uongozi shuleni hapo. Shida ni msichana mwenye umri wa miaka 18 – 20
ambaye alikuwa hajawahi kupata stadi za maisha ila alikuwa ni mtu mwenye
kujielewa kama yeye ni nani, yupo wapi na anakwenda wapi, pamoja na kujisamini
katika maisha yake na vile vile ni mtoto mwenye kumjali na kumsamini kila mtu
mkubwa ama mdogo. Alikuwa na uwelewa mkubwa sana katika hali ya kufafanua mambo
tofauti hususa ya kimapenzi kwani hukutamani hata siku moja kijiingiza katika
msukumo wa mapenzi. Lakini shoga yake Shida na yeye alikuwa ni msichana mwenye
kukadiriwa kuwa na umri sawa sawa na wa Shida kati ya miaka 18 – 20 ambao
ukiwaona utazania kama mapacha ila yeye tayari ameshashawishika na kijiingiza katika
masuala ya kimapenzi akiwa yupo katika umri mdogo sana. Hata hivyo Shida
alichukua jitihada kubwa kumsemeza shoga yake ili aachane na mapenzi.
Shida alifurahiya sana maisha yake ya sasa pamoja na
kuonyeshwa upendo na mapenzi mazuri kutoka kwa wazazi ama walezi wake pamoja na
kupatiwa huduma zote za kimahitaji zidi yake kama vile chakula, mavazi mazuri
na malazi bora hayo yote yalikuwa kutoka kwa wazazi wa shoga yake. Kama ilivyo
kwa jamiina kusema rafiki mwema ni mwenye kuijenga familia. Kwani hata yeye
alijitahidi kuonesha hali ya upendo zaidi na aliwaona kama wazazi wake,
aliwaheshimu na kuwasamini na kuwasikiliza kwa kila jambo na yote yale ambayo
atakayo amrishwa kwake. Alipendelea sana kufanya Ibada na kumuhimiza Shoga yake
katika kufanya Ibada na kumuomba Mungu wake katika kila kitu kwani ndio
kiongozi wake wa kila siku. Shida alianza kujiwekea malengo makubwa sana katika
maisha yake. Miongoni mwa malengo ya shida ni kuwa mmoja kati ya wanawake wenye
kuwakilisha wanawake wenzake katika jamii. Shida alipata nafasi ya kuwa mwenye
kusikilizwa kwa wazazi aliokua anaishi nao, Siku zilizidi kwenda katika
harakati za kutafuta elimu kwa Shida hadi siku moja Shida akiwa anaelekea kumaliza
elimu yake ya sekondari. Shida alifanikiwa na kujiendeleza kimasomo katika
nyanja mbali mbali na sehemu tofauti. Hata muda ulipotimia kumaliza kwa masomo
yake, Shida aliona ni bora kuanza kuhangaikia masuala ya kutafuta kazi. Kwa
bahati nzuri Shida alipata nafasi ya kuajiriwa katika offisi moja inayoshuhulikia masuala ya Amani
na Upendo katika nchi, ambako ndani ya offisi hiyo anabahatika kukutana
na mvulana mwenye mvuto wa kimapenzi na kuanza kupendana. Ni siku ya kwanza kwa
Shida kuanza kujiingiza katika masuala ya kimapenzi, ila hakuwa na niya mbaya
kwani kila mmoja wao alikuwa na niya nzuri tu haswa katika kutimiza moja kati
ya lengo lao la kufunga ndoa (kuowana).
Siku nenda siku rudi na muda kupita, Shida alibahatika kuwa
ni mwenye kumiliki sehemu yake mwenyewe ya kukaa na kujiendeleza kimaisha, yani
alipata nyumba yake binafsi na ndipo alipoona kuwa kuna umuhimu mkubwa wa
kumiliki familiya yake. Baada ya kuwa na
hali hii aliwaomba wazazi ambao aliokuwa anaishi nao ili aweze kuhama nyumbani pale na kwenda kuanza
kuishi maisha yake mapya katika nyumba yake binafsi iliyopo mbali kidogo na mji
waliokuwa wanaishi wazazi wa shoga yake ambao ndio wazazi wake pia kwa sasa.
Shida alikubaliwa na alianza kuishi katika nyumba yake.
Tukirudi katika maisha ya nyuma ya enzi za Mr.Jongo ambaye ni
mjomba wake na Shida anapata tatizo la
kutokuwa na fahamu baada ya kupatwa na ajali mbaya sana akiwa anarudi katika
mahangaiko yake usiku wa manane kama kawaida yake na huku akiwa amelewa
chilalila hajiwezi mkono wala mguu, baada ya kumaliza bara bara ya kwanza na
anaingia ya pili ilikatiza gari na kumgonga kwa kasi na kwa wakati ule wa usiku
hapakuwa na msaada wa kutosha kwani kila mtu alikuwa yupo nyumbani kwake
amelala na hadi katika majira ya usubuhi ndipo wasamaria wema kumuona akiwa
hali mbaya sana na ndipo alihaishwa hospitali mapema na asubuhi hiyo hiyo baada
ya kupatiwa matibabu alionekana kuwa ni mtu mwenye hali ya kawaida na ndipo
alipelekwa nyumbani kwake kuugulia, kiukweli aliumia sana sehemu za kichwa na
kupoteza damu nyingi sana na ndo sababu iliyopelekea kupeteza kwa maisha yake
ila kabla mauti hayajamkuta na baada ya kuona hali inazidi kuwa ngumu ilibidi
habari ya ugonjwa wake itangazwe katika vyombo vya habari ili kumfikishia mtoto
wao Shida popote pale alipo. Shida baada ya kupata taarifa ya mjomba wake
ilibidi kuelekea kijiji kwao kwa ajili ya kumumgulia hali mjomba wake, habari
ya kusikitisha kwa Shida ilianzia katika safari yake kwani kabla Shida hajafika
akiwa ndani ya basi anapata habari ya msiba wa mjomba wake Mr. Jongo,
ukitangaziwa katika basi alilopanda. Shida unauwahi msiba na kushuhudia maziko
ya mjomba wake na baada ya kumalizika kwa msiba watu wanachawanyika na kila mtu
kuelekea nyumbani kwake na Shida na yeye anaona ni bora kumliwaza Shangazi yake
na vile vile kumtaka kumchukuwa katika nyumba anayo ishi yeye, baada ya
kukubaliana na kuamua kuondoka Shida anaongozana na familiya ya marehemu kwenda
kuishi nao pamoja. Shida anafika nyumbani kwake na aliyekuwa mke na mjomba yake
pamoja na watoto wake na kuanza maisha mapya.
Leo ni Siku ya tarehe 26/7 Kuzaliwa kwa Shida “happy birthday”
“to Shida” watu wote walianza kuandaa mazingira mazuri ya matayarisho ya “happy
birthday kwa Shida” yalianza mapema kwa ajili ya kufurahiya siku ya kuzaliwa
kwake na kuanzia nyumbani kwake na kuelekea katika ukumbi mmoja maarufu sana
unaojulikana kwa jina la “SANTINA HALL” ambao upo katikati ya mji huo. Ikiwa
ndugu na jamaa wa Shida wameshafika katika ukumbi wa shughuli pamoja na
majirani zake, vile vile na mashoga zake
nao wakiwa wameshahudhuria katika sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa Shida yani
“happy birthday to her” Watu wake wa karibu sana pamoja na wageni mbali mbali
walikaribashwa na kupokewa vizuri. Walianza kupata vyakula na vitu mbali mbali
pamoja na kunywa vinywaji tofauti na vile vile wakifurahia kwa kucheza mziki wa
aina tofauti hadi ilipofika zamu ya kutoa na kupotea zawadi. Ikiwa sasa ni zamu
ya upokeaji wa zawadi kwa Shida kutoka kwa rafiki zake na shoga zake pamoja na
watu tofauti waliohudhuria katika hall hilo, sherehe ziliendelea vizuri tu hadi
pale Shida alipokuwa yupo tayari kupokea zawadi, Shida aliambiwa asimame kwa
kupokea zawadi na alianza kupokea kutoka kwa jamaa zake na kumalizia kwa watu
wengine. Ni baada ya mapumziko mafupi ya kumaliza upokeaji wa zawadi kwa Shida
kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki. Na sasa ni wakati wa kupokea zawadi kutoka
kwa mchumba wake ilitangaziwa sasa ni zamu ya Shida kupokea zawadi kutoka kwa
Mchumba wake. Kila mtu alikua na hamu ya kumuona mchumba wa Shida na jee ni
zawadi gani ya kipekee atampa Mchumba wake “Shida”. Na jee Shida ni nini
atapokea kutoka kwa mchumba wake?.
Mchumba wa Shida
alikua na hamu ya kufanya maamuzi ya kipekee katika shughuli hii na alitaka
kila mtu ajue ni jinsi gani anavyompenda mchumba wake. Alikua na mkoba mdogo
sana katika mikono yake na alipanda juu ya Stage na aliamuwa kukaa chini na
kufungua zipu huku akiwatazama watu waliokuwa katika hall hilo. Chaajabu nacho
na watu wote walimtazama yeye jee sasa atafanya nini baada ya kufungua zipu? Mchumba
wa Shida Alitoa box la saizi liililofungwa na kuzungurushwa kwa gift paper,
aliamua kumuita mchumba wake karibu yake na kumfungulia box lile ili apate
kujionea mwenyewe. Baada ya kufungua na kuona kilichomo ndani yake. Duh! Ilikua
ni ajabu kubwa sana kwa Shida, huwezi kuamini kwa haya kumbe ni zawadi hii:
kwani mulikuwa na :- “MKATE WA BOFLO”
watu wote hoi! Walicheka na kunong’onezana huku wakisema aibu gani hii
ameshamfanyia mwenzake? Wakiwa wanaendelea kumsema mchumba wake Shida walisema
hivi “kwani haoni kuwa sote hapa tumekuja na vitu vizuri vya kumpa Shida katika
siku yake hii”. Hafla walishangaa kumuona Shida ana furaha kubwa iliyopindukia
mipata kwa kuona zawadi ya Mkate wa boflo, Shida aliona hii yote ni ishara ya
upeno zidi yake, ikiwa Shida yupo katika furaha ndani ya furaha yake lilimjia
lepelepe la kumbukumbu. Alikumbuka maisha yake ya mwanzo katika kipindi cha
Wazazi wake, pamoja na pale ambapo alipowapowateza wazazi wake, alikumbuka na
pale ambapo alipo kwenda kuishi kwa mjomba wake Mr. Jongo. Alikuwa na maisha
magumu sana kipindi kile, sasa leo hakuwa na tatizo la kutopotea zawadi mkate
wa boflo, kwani aliamini kuwa zawadi ni zawadi tu, na ndipo alipomkimbilia mchumba
wake na kumkumbakia na kumbusu mabusu mengi mengi kama mvua, watu wote
walichukia sana kitengo kile na hali ya kuwa Shida akiwa na furaha. Lakini
baada ya muda mfupi mchumba wa Shida alimtuliza Shida kutoka katika furaha na
kumuweka katika hali yake ya kawaida na kuwataka watu wote kushuhudia ukatwaji
wa Mkake, aliukata mkate ule kwa kisu ambacho kilikatiwa keki, aliukata kati na
kati na kumbe ndani ya Mkate wa Boflo ule mulikuwa na maajabu makubwa na
yakushangaza na kustaajabisha watu wote.
Ndani ya mkate ule mulikuwa na:- Mkufu wa Dhahabu Wenye Thamani ya Pesa
Taslimu ya Milions Nane za Kitanzania na Pete ya Kudhihirisha Uchumba wao pamoja na Ufunguo wa Gari aina ya “NADIA” ambavyo vitu hivi vyote
alikabidhiwa Shida na Mchumba wake kuwa ni zawadi yake katika siku yake ya
kuzaliza. Shida hakuamini machoni mwake aliruka na kumkumbatia kwa furaha kubwa
sana.Watu wote hawakuamini kama kweli duniani kuna watu wana moyo wa imani kama
huyu kaka, kiukweli ilikua ni siku ya aina yoke kwa Shida. Kila mmoja wao
alitamani kuwa yeye kama Shida ila yote ni majaaliwa ya Mungu. Baada ya
kumalizika shughuli ambayo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Shida watu wote
walichawanyika na kila mtu kurudi nyumbani kwao. Baada ya kila mtu kufika
nyumbani kwao, kwani kila mtu alikuwa na mawazo tofauti kuhusu siku hii. Shida
pamoja na mchumba wake waliamuwa kuandaa mikakati ya kufunga ndoa, walichukua
hatua ya kuwajuulisha wazee, ndugu na jamaa. Mikakati ya harusi ikiwa ipo
katika maandalizi mazuri, Shida alimpeleka mchamba wake kwa wazazi wa shoga
yake ambao wamemlea na kama ni wazazi wake waliopo akiambatana na shangazi yake
ambae alikuwa ni mke wa mjomba wake marehemu Mr. Jongo, ila kwa upande wa
wazazi hao walichukuwa hatua ya waliasiliana na jamaa pamoja na ndugu wa wazazi
wake walioko ambao wanaishi “ukerewe
kisiwani” katika ziwa la Victoria mkoani mwanza, Shida ilibidi apelekwe huko
kwa ajili ya kufanyiwa maandalizi ya harusi yake kama ilivyo kawaida na desturi
zao. Shida alikuwa tayari kwenda kusubiri harusi yake huko kisiwani na vile
vile alimpa taarifa mchumba wake kuwa harusi yao inatarajiwa kufanyika huko
kisiwani, kwani haikuwa tabu sana kwa watu wawili hao na ndipo Shida alipowasilishwa
kisiwani huko. “Ukerewe”Siku ya harusi ilipofika iliandaliwa kamati ya
watu wasiopungua takribani kumi na mbili akiwemo na bwana harusi mtarajiwa
kuelekea harusini kwenda kumuoa Shida na kuwa mke wake wa ndoa. Baada ya kufika
kivuukoni walipokewa na wenyeji wao waliokuwa wanawasubiria kivuukoni hapo na
wakaendelea na safari yao. Ila chakushangaza zaidi ni pale waliopokaribia
kumaliza kuvuuka ziwa hilo kwa kutumia dau aina ya “Mtumbwi”. Mmoja kati
ya mwenyeji wao aliwambia baadhi ya masharti ya kisiwa hicho, aliwambia kuwa “Mnapokuwa
njiani siruhusa kuzungumza na mwenzio wala kugeuka nyuma mara mara na chochote
mtakachokiona njiani musioneshane na kumwambia mwenzio hadi pale mtakaporudi
katika mji wenu na nimarufuku kutoka nje wakati wa usiku”. Kiukweli waliwekwa
katika hali ngumu sana ila walipiga moyo konde kuwa yote ni safari.
Baada ya kufika kisiwani huko walishangazwa sana kutomuona
msichana hata mmoja katika kijiji hicho, isipokuwa wazee tu. Na chakushangaza
zaidi lengo ni kwenda kuowa ila kulikuwa kimya na hakuna harakati zozote za
harusi, lakini walipokelewa vizuri na kukaribishwa vyema. Zilipita siku mbili -
tatu hawakuona harusi wala biharusi mwenyewe, baada ya muda mfupi walipata
taarifa mbaya sana kwa Shida. Waliambiwa kuwa Shida anaumwa sana na harusi itabidi
ihairishwe. Waliongozona na kwenda kumuona Shida nyumbani kwa bibi yake, Shida
alikuwa ameoza mkono na amefanya shimo katika sehemu ya paja lake, mchumba wake
Shida alihuzunika sana na kuhairisha harusi yao hadi pale hali ya Shida
itakapokuwa sawa. Ilibidi waanze maandalizi ya kurudi nyumbani kwao na kumuacha
Shida akiuguza ugonjwa wake, walitembezwa na kuwaaga wanakijiji hadi katika
nyumba ya babu yake shida na waliambiwa wachukuwe zawadi ya kuku, walioneshwa
chumba kimoja ili wafunguwe na wachukuwe kuku waliyokuwemo ndani ya chumba
hicho na mlikuwa na kuku wawili tu. Walishangazwa sana baada ya kuwaona kuku
waliokuwemo ndani ya chumba hicho kwani kuku hao walikuwa wanaukubwa kama kinda
la ng’ombe (Ndama). Walibana mlango kwa kasi na kudai eti wao hawataki
kuchukuwa zawadi.
Walikunja virago vyao na kurudi mjini na baada ya kuhairisha
kwa harusi walioikusudia. Baada ya kufika mjini mambao yalikuwa tafrani katika
majumba yao hali ya kuwa kila mzee alipandisha mashetani na walizidi kuchagawa
na huku wakisema wameenda kuchukuwa matatizo kisiwani huko. Baada ya wiki mbili,
tatu ilitokea taarifa mbaya sana kwa jamii kupitia vyombo vya habari “Shida
amefariki dunia na kupoteza maisha yake” ni hali ya kuhuzunisha kwa watu wote hususani
kwa yule wa moyoni mwake ambaye alikuwa mchumba wake. Inavyosemekana Shida nae
amekufa na kuchukuliwa kiuchawi. Baada
ya kusahaulika kwa msiba wa Shida na mchumba wake Shida aliugua wazimu na
kupelekea kuwa Chizi kwa ajili ya
kumkumbumba mchumba wake Shida na vile vile alipoelezwa na kujua kwa nini akaitwa “Shida”
kabla ya ugonjwa kumvaa alisimuliwa “historia fupi ya Shida na kuhusu wazazi
wake” Duh! Alihuzunika sana na ndipo alipojuaa kuwa wale kuku waliokuwa wataka
kupewa zawadi kule kisiwani kumbe walikuwa ni wazazi wake Shida ambao waliwekwa
kiuchawi na walihifadhiwa kwa njia ya ushirikina. Alizidi kusimuliwa kuhusu
wazazi wa Shida kabla hawajapotea katika hali hatarishi, aliambiwa kuwa kipindi
ambacho alizaliwa Shida ilikuwa ni kipindi cha shida na matatizo kwa wazazi
wake na ndio maana wakaamua kumuita mtoto wao Shida kutokana na shida
waliokuanayo, hawakujua kama jina litaweza kumsibu mtoto wao.
Na kwa kweli Shida jina limemsibu, kwani tangu anazaliwa hadi
anakufa aliishi katika maisha ya shida kwani alizaliwa na shida na alikufa na
shida. Kwake ilikuwa ni maisha ya shida. Mchumba wa Shida alichanganyikiwa sana baada
ya kujua na kuelewa hali halisi iliyokuwa ya maisha ya Shida kipindi cha uhai
wake. Na ndipo pale alipochanganyikiwa na kupoteza fahamu zake hali hii
ilimpelekea kuugua Uwandawazimu (Uchizi).
Kiukweli ilikuwa ni hali ya kuhudhunisha na kusikitisha
ambayo imesababisha kuleta majuto na matatizo na ilikuwa ni shida kumfaham
Shida katika maisha yake. Ilibidi achukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya
wagonjwa wa akili (Mental) Milembe
Mkoani Dodoma.
MWISHO WA
SIMULIZI
MTUNZI
MOHAMED HEMED ISSA (BIZOMAN.COM)
SPONSOR BY: TANZANIA
YOUTH ICON (TAYI)
Wasiliana
Simu Namba: +255(0) 773 450 2324/ +255(0) 655 450 234
Facebook tafuta: Mohammed Issa (pofile online)
What`sApp tafuta: Eddiey Bizo on 0655450234
E-mail
yangu: eddieyissa@gmail.com
No comments:
Post a Comment