KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Tanzania mwaka 2015/2016,
Juma Khatib Chum, akimkabidhi chandarua mtoto Fatmat Abdalla Mohammed,
anayeishi na VVU mara baada ya kuonyesha hali halisi ya maisha yake katika
kituo cha Ushauri nasaha ZAPHA+ mkabala na ofisi ya Halmashauri ya Chake Chake
Pemba.
MKUU wa Wilaya ya Mkoani isiwani Pemba Mhe:Hemed Suleiman
Abdalla, akipima afya katika banda la ushauri nasaha linalomilikiwa na ZAPHA+
katika mkesha wa mwenge wa uhuru Tanzania Chake Chake Pemba.
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Pemba Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud,
akimkabidhi Risala ya wananchi wa Chake Chake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru kitaifa Juma Khatib Chum, kwa lengo la Kwenda kumkabidhi Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla wapili
kutoka kulia, katikati ni Kiongozi wa wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu
Juma Khatib Chum, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe:Hanuna
Ibrahim Massoud akiwa na wakimbizaji wa mwenge wa uhuru pamoja na Mkuu wa
Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla.
No comments:
Post a Comment