Balozi Seif Ali Iddi Azindua Kampeni za CCM Jimbo la Kikwajuni.
Balozi
Seif akimnadi mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kikwajuni kwa Tiketi ya
Chama cha Mapinduzi Mhandisi Hamad Masauni Yussuf.
Balozi
Seif akimnadi mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Jimbo la Kikwajuni Nd. Nassor Salim Ali
Jazira.
Balozi
Seif akiwakabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Ndugu Mbarouk Abdulla Hanga
wa kwanza kutoka kushoto anayewania Udiwani Wadi ya Rahaleo na Nd.
Ibrahim Khamis Fataki Ngasa Udiwani Wadi ya Kikwajuni kwa tiketi ya CCM
(PICHA NA EDDIEY BIZO)
Vijana
wa Mjini wakiserebuka wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya
Uchaguzi ya Jimbo la Kikwajuni ilyofanyika Miembeni Jitini Mjini
Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya
CCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi..
(PICHA NA EDDIEY BIZO)
Na.Othman Khamis OMPR
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kampeni ya Uchaguzi ya CCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema kwamba wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wana kila sababu ya
kuwaunga mkono Viongozi waliothibitishwa na CCM kugombea nafasi za
Uongozi wa Jimbo hilo ili liendelee kuongozwa na chama hicho.
Balozi
Seif alisema Viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na lile lililokuwa Rahaleo
walifanya kazi kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika
kusimamia Maendeleo ya Wananchi wa Majimbo hayo walipojizatiti
kukabiliana na matatizo ya Kijamii.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizindua Rasmi Kampeni ya Uchaguzi
ya Jimbo la Kikwajuni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mkutano
uliofanyika katika uwanja wa Miembeni Jiti kubwa Mjini Zanzibar.
Alisema
changamoto ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama ilipunguwa
kwa kiasi kikubwa ndani ya Majimbo hayo kutokana na umahiri mkubwa
ulioonyeshwa na Viongozi hao katika kuwatumikia wananchi wao ndani ya
kipindi hicho cha miaka mitano.
NA WATAISOMA NAMBA
1 comment:
Mara hii juu kwa juu
Post a Comment