Saturday, September 19, 2015

TUMEAHIDI, TUMETIMIZA, SASA MBELE KWA MBELE

Balozi Seif Ali Iddi Azindua Kampeni za CCM Jimbo la Kikwajuni.

Balozi Seif akimnadi mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kikwajuni kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhandisi Hamad Masauni Yussuf.
 Balozi Seif akimnadi mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Jimbo la Kikwajuni Nd. Nassor Salim Ali Jazira.
 Balozi Seif akiwakabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Ndugu Mbarouk Abdulla Hanga wa kwanza kutoka kushoto anayewania Udiwani Wadi ya Rahaleo na Nd. Ibrahim Khamis Fataki Ngasa Udiwani Wadi ya Kikwajuni kwa tiketi ya CCM
(PICHA NA EDDIEY BIZO)
Vijana wa Mjini wakiserebuka wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Uchaguzi ya Jimbo la Kikwajuni ilyofanyika Miembeni Jitini Mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi..
(PICHA NA EDDIEY BIZO)

Na.Othman Khamis OMPR 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Uchaguzi ya CCM  Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alisema kwamba wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wana kila sababu  ya kuwaunga mkono Viongozi waliothibitishwa na CCM kugombea nafasi za Uongozi wa Jimbo hilo ili liendelee kuongozwa na chama hicho.

Balozi Seif alisema Viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na lile lililokuwa Rahaleo walifanya kazi kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika kusimamia Maendeleo ya Wananchi  wa Majimbo hayo walipojizatiti kukabiliana na matatizo ya Kijamii.

Balozi Seif  Ali Iddi alisema hayo wakati akizindua  Rasmi Kampeni ya Uchaguzi ya Jimbo la Kikwajuni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi  Mkutano uliofanyika katika uwanja wa Miembeni Jiti kubwa Mjini Zanzibar.

Alisema changamoto  ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama ilipunguwa kwa kiasi kikubwa ndani ya Majimbo hayo kutokana na umahiri  mkubwa ulioonyeshwa na Viongozi hao katika kuwatumikia wananchi wao ndani ya kipindi hicho cha miaka mitano.
 
NA WATAISOMA NAMBA

1 comment:

Unknown said...

Mara hii juu kwa juu