Innaa Lillaahi Wainnaa ilayhi Raaji'uun : Zaidi ya Mahujaaj 200 wafariki leo wakati wakijiandaa kurusha vijiwe
Kiasi cha Mahujaaj wanaozidi 200
wamefariki asubuhi ya leo wakati walipokuwa wakielekea kwenye sehemu ya
kurusha Vijiwe eneo la Mina nje kidogo ya Mji wa Makkah.
Mahujaaj wengine zaidi ya 400 pia
walijeruhiwa wakati lilipotokea tukio hilo la mkanyagano wakati
walipokuwa wakiingia katika moja ya (Tunnel) walipokuwa wakitoka Mina
kuelekea eneo la Jamaraat ( kurusha vijiwe).
Eneo la kurusha vijiwe bado ni eneo
la hatari sana kutokea mkanyagano licha ya kutanuliwa na kuwekewa
utaratibu mzuri wa kurusha vijiwe na Serikali ya Saudia.
Mpaka tunapoituma taarifa hii
hatujapata taarifa zozote kwamba katika miongoni mwa waliotangulia mbele
ya haki kuwamo Mahujaaj kutoka nyumbani.
Mola awasamehe madhambi yao, awarehemu kwa rehma yake na awaingize katika Jannatul Firdaus. Aamiyn
No comments:
Post a Comment