Dk Shein Mgeni Rasmin Fainali za Mchezo wa Bao na Karata Viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya
Ekrotanali maisara kuhudhuria Fainali ya michezo ya Bao na Karata
akiongozana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Sharifa Khamis.
Washiriki wa michezo ya fainali ya Bao
na Karata wakiwa katika viwanja vya mchezo huo kabla ya kuaza kwa
fainali ya Uzinduzi wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kwa mchezo wa Bao.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo
Zanzibar Ndg Khamis Andalaa akitowa maelezo ya kuchuano ya Fainali ya
michezo ya Bao na Karata ilizishirikisha Timu 8 Nne kutoa Unguja na
Pemba kwa mchezo wa Bao na mchezo wa karata ili kumpata bingwa wa
michezo hizo Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akifuatilia maelezo ya ufunguzi wa
michezo ya fainali ya mchezo wa Bao na Karata katika viwanja vya
Ekrotanali maisara Zanzibar. kushoto Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Utalii na Michezo Mhe Bihindi Hamad na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Mhe Abdalla Mwinyi Khamis.
Mwakilishi wa Mchezo wa Bao akisoma
kanuni za mchezo huo kabla ya kuaza kwa fainali ya mchezo huo
uliwakutanicha wachezaji wa Timu ya Muembeladu Ndg Kididi Salum Kidodi
na Mchezaji wa Timu ya Jangombe Ndg Omar Othman, katika mchezo huo wa
Bao Kidodi Salum Kidodi ameibuka mshindi wa 2--1.
Msimamizi wa fainali ya mchezo wa Karata
akisoma kanuni za mchezo huo wa fainali kabla ya kuaza mchezo huo
uliozikutanisha timu za Kibanda Mawazo ya Wawi Chakechake Pemba na Timu
ya Kilimahewa Star, timu ya Kibanda Mawazo kutoka Pemba imeshinda mchezo
huo kwa mizinga 4-2.
Baadhi ya Washiriki wa michezo ya Fainali ya Bao na Karata wakiwa katika viwanja vya michezo hiyo Ekrotanali Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizindua michezo ya Fainali ya Bao
na Karata kwa mchezo wa Bao, akicheza na Ndg Abdalla Salum Kitambo, ukiwa mchezo wa ufunguzi wa fainali hizo katika mchezo huo.Dk Shein amefunga bao 1--0.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi akionesha ufundi wa kusafiri kupitia mchezo wa bao wa
ufunguzi wa fainali ya michezo ya Bao na Karata iliofanyika katika
viwanja vya Ekrotanali maisara Zanzibar katika mchezo huo Dk Shein,
amefungwa bao moja na Ndg Abdalla Salum Kitambo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi akionesha ufundi wa kusafiri kupitia mchezo wa bao wa
ufunguzi wa fainali ya michezo ya Bao na Karata iliofanyika katika
viwanja vya Ekrotanali maisara Zanzibar katika mchezo huo Dk Shein,
amefungwa bao moja na Ndg Abdalla Salum Kitambo.
Baadhi ya Wapenzi wa mchezo wa Bao na
Karata Zanzibar weakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa Fainali ya michuano
hiyo iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Ndg Abdalla Salum
Kitambo kwa ushindi wa mchezo huo wa ufunguzi wa mchezo wa bao wakati wa
michuano ya fainali iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.
Mchezo wa fainali ya Bao kati ya Kidodi
Salum Kidodi na Omar Othman ukipamba moto kutafuta bingwa wa mchezo huo
Zanzibar, kila mtu akionesha ufundi wake wa bao la kete. mchezo huo
umefanyika katika viwanja vya Ekrotanali maisara Zanzibar kulia Bingwa
wa Mchezo huo Ndg Kidodi Salum Kidodi na kushoto Ndg Omar Othman.
mshindi wa Pili wa Mchezo wa Bao Zanzibar.
Bingwa Kidodi akipiga hesabu za mchezo
huo kabla ya kuaza kucheza katika kipindi hicho wate wakiwa sare ya bao
1-1.na muamuzi wa mchezo huo akifuatilia bila ya kuonesha upendeleo kwa
mchezaji yoyote katika mchezo huo wa fainali.
Ndg Kidodi akisafiri kupia mchezo ya bao kutafuta ushindi dhidi ya mpinzani wake Ndg Omar Othman.
Mchezo wa fainali wa Karata kati ya Timu
kutoka Wawi Pemba ya Kibanda Mawazo na Timu kutoka Unguja ya Kilimahewa
Star, ukipamba moto wakati wa fainali yao ya kutafuta bingwa wa
Zanzibar wa mchezo wa Karata Zanzibar.
Maguji wa mchezo wa Karata kutoka Pemba
na Unguja wakioneshana ufundi wa mchezo huo wa wahedi wasitini
uliozikutanisha timu za Kibanda Mawazo ya Wawi Chakechake iliibuka
Bingwa wa Mchezo huo kwa kuifunga Kilimahewa Star. kwa mizinga 4-2.
Baadhi ya wapenzi wa michezo ya Bao na
Karata wakifuatilia fainali hizo za kutafuta Bingwa wa Zanzibar kwa
michezo ya Asili Zanzibar hususan kwa Bao na Karata hupendwa sana
Zanzibar.
Wapenzi wa mchezo wa Bao na Karata wakifuatilia michuano hiyo ya fainali katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar
Sharifa Khamis akizungumzia michuano hiyo ya fainali ya michezo Bao na
Karata iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar. mgeni rasmin
akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali
Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa Mchezo wa Karata na Bao
Zanzibar akisoma risala ya michuano hiyo wakati wa fainali zake
zilizofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar kwa kuzikutanisha
timu kytoka Unguja na Pemba katika michuano ya fainali na kuto shukrani
kwa mashirika yaliofanikisha michuano hiyo tangu mwazo hadi mwisho wa
michuano hiyo na kupatika Bingwa wa michezo hiyo Zanzibar katika viwanja
vya Ekrotanali Zanzibar.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii
na Michezo Zanzibar Bihindi Hamad akizungumza wakati wa michezo ya
fainali ya Bao na Karata katika viwanja vya Ekrotanali na kumkaribisha
mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Ali Mohamed Shein.
Viongozi wa Serikali wakimsikiliza Rais
wa Zanzibar Dk Shein, akizungumza na wanamichezo ya Asili Zanzibar
wakati wa fainali ya michezo hiyo iliofanyika katika viwanja vya
Ekrotanali maisara Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wanamichezo wa
michezo ya Bao na Karata Zanzibar wakati michuano wa michezo ya fainali
iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar na kupatikana
mabingwa ni michezo hiyo.
Washiriki wa michuano ya mchezo wakarata wakimsikiliza Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
Mshiriki wa mchezo wa Fainali ya michuano ya Bao na Karata akitowa
shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa
Mchezo wa Bao Zanzibar Ndg Kidodi Salum Kidodi kwa kumshinda mpizani
wake kutoka Jangombe Ndg Omar Othman kwa Bao 2-1, katika mchezo wa
fainali uliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali na kukabidhiwa Kombe
na Fedha taslim shilingi laki tano.
Bingwa wa Zanzibar wa Mchezo wa Bao Ndg Kidodi Salum Kidodi akifurahia ubingwa wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi mshindi wa Pili wa
Mchezo wa Bao Ndg Omar Othman Kombe na fedha taslim shilingi laki Tatu.
No comments:
Post a Comment