Rais wa Marekani Barack Obama
amezungumza na mwenzake wa Cuba Raul Castro kwa njia ya simu, muda mfupi
baada ya marekani kutangaza kuwa imelegeza vikwazo vya kiuchumi dhidi
ya kisiwa hicho.
Kuanzia siku ya Jumatatu makampuni fulani nchini
Marekai kwa mara ya kwanza yataanza kufanya ushirikiano na makampuni ya
Cuba na kufungua ofisi nchini humo.
Vikwazo vya usafiri pia navyo vimelegezwa kwa raia wa marekani.
Rais
Castro amezungumzia haja ya kuondolewa kwa vikwazo vyote, lakini bado
hajasema ikiwa ataruhusu makampuni ya Marekani kama Mcdonalds na
Starbucks kufungua biashara nchini Cuba.
No comments:
Post a Comment