Kumekuwa na dalili za kuongezeka
misukosuko kati ya nchi za ulaya, wakati zinapojaribu kukabiliana na
maelfu ya wahamiaji na wakimbizi wanaojaribu kufika kaskazini na
magharibi mwa ulaya.
Hungary umemlaumu jirani wake Croatia kwa
kukiuka sheria za kimataifa na kushiriki katika ulanguzi wa watu, baada
ya utawala nchini croatia kuanza kusafirisha wahamiaji kwenda nchini
Hungary bila kuwaandikisha.Akiongea na BBC waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Croatia Vesna Pusic, ametaka kuwepo hatua za pamoja kutatua suala hilo na kujumuisha nchi zote za ulaya na nchi majirani.
No comments:
Post a Comment