Monday, September 28, 2015

ZEC YAFANYA SEMINA JUU YA SUALA ZIMA LA KUGIPA KURA

ZEC yaendesha semina kwa watendaji wa vituo vya ugawaji wa shahada za kupigia kura

DSC03427
Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Magharib Ndg Ali Rashid Suluhu akiwasilisha mada katika mafunzo ya watendaji wa vituo vya Ugawaji wa Shahada za kupigia Kura, mafunzo ambayo yalifanyika ukumbi wa Skuli ya Mwanakwerekwe ”C” tarehe 26/09/2015
DSC03433
Washiriki wa semina ya watendaji katika vituo vya Ugawaji shahada za kupigia Kura wakimsikiliza kwa makini Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Magharib Ndg Ali Rashidi Suluhu wakati akiwasilisha mada katika mafunzo hayo ambayo yalifanyika ukumbin wa skuli ya Mwanakwerekwe ”C” tarehe 26/09/2015. Mafunzo kama hayo yalifanyika kwa wilaya zote za Unguja na Pemba.

Dk Shein Mgeni Rasmin Fainali za Mchezo wa Bao na Karata Viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Ekrotanali maisara kuhudhuria Fainali ya michezo ya Bao na Karata akiongozana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Sharifa Khamis. 

Washiriki wa michezo ya fainali ya Bao na Karata wakiwa katika viwanja vya mchezo huo kabla ya kuaza kwa fainali ya Uzinduzi wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kwa mchezo wa Bao.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Ndg Khamis Andalaa akitowa maelezo ya kuchuano ya Fainali ya michezo ya Bao na Karata ilizishirikisha Timu 8 Nne kutoa Unguja na Pemba kwa mchezo wa Bao na mchezo wa karata ili kumpata bingwa wa michezo hizo Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akifuatilia maelezo ya ufunguzi wa michezo ya fainali ya mchezo wa Bao na Karata katika viwanja vya Ekrotanali maisara Zanzibar. kushoto Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Bihindi Hamad na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis.
Mwakilishi wa Mchezo wa Bao akisoma kanuni za mchezo huo kabla ya kuaza kwa fainali ya mchezo huo uliwakutanicha wachezaji wa Timu ya Muembeladu Ndg Kididi Salum Kidodi na Mchezaji wa Timu ya Jangombe Ndg Omar Othman, katika mchezo huo wa Bao Kidodi Salum Kidodi ameibuka mshindi wa 2--1.
Msimamizi wa fainali ya mchezo wa Karata akisoma kanuni za mchezo huo wa fainali kabla ya kuaza mchezo huo uliozikutanisha timu za Kibanda Mawazo ya Wawi Chakechake Pemba na Timu ya Kilimahewa Star, timu ya Kibanda Mawazo kutoka Pemba imeshinda mchezo huo kwa mizinga 4-2.

Baadhi ya Washiriki wa michezo ya Fainali ya Bao na Karata wakiwa katika viwanja vya michezo hiyo Ekrotanali Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizindua michezo ya Fainali ya Bao na Karata kwa mchezo wa Bao, akicheza na Ndg Abdalla Salum Kitambo, ukiwa mchezo wa ufunguzi wa fainali hizo katika mchezo huo.Dk Shein amefunga bao 1--0.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akionesha ufundi wa kusafiri kupitia mchezo wa bao wa ufunguzi wa fainali ya michezo ya Bao na Karata iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali maisara Zanzibar katika mchezo huo Dk Shein, amefungwa bao moja na Ndg Abdalla Salum Kitambo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akionesha ufundi wa kusafiri kupitia mchezo wa bao wa ufunguzi wa fainali ya michezo ya Bao na Karata iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali maisara Zanzibar katika mchezo huo Dk Shein, amefungwa bao moja na Ndg Abdalla Salum Kitambo.
Baadhi ya Wapenzi wa mchezo wa Bao na Karata Zanzibar weakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa Fainali ya michuano hiyo iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Ndg Abdalla Salum Kitambo kwa ushindi wa mchezo huo wa ufunguzi wa mchezo wa bao wakati wa michuano ya fainali iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.

Mchezo wa fainali ya Bao kati ya Kidodi Salum Kidodi na Omar Othman ukipamba moto kutafuta bingwa wa mchezo huo Zanzibar, kila mtu akionesha ufundi wake wa bao la kete. mchezo huo umefanyika katika viwanja vya Ekrotanali maisara Zanzibar kulia Bingwa wa Mchezo huo Ndg Kidodi Salum Kidodi na kushoto Ndg Omar Othman. mshindi wa Pili wa Mchezo wa Bao Zanzibar.

Bingwa Kidodi akipiga hesabu za mchezo huo kabla ya kuaza kucheza katika kipindi hicho wate wakiwa sare ya bao 1-1.na muamuzi wa mchezo huo akifuatilia bila ya kuonesha upendeleo kwa mchezaji yoyote katika mchezo huo wa fainali.

Ndg Kidodi akisafiri kupia mchezo ya bao kutafuta ushindi dhidi ya mpinzani wake Ndg Omar Othman.

Mchezo wa fainali wa Karata kati ya Timu kutoka Wawi Pemba ya Kibanda Mawazo na Timu kutoka Unguja ya Kilimahewa Star, ukipamba moto wakati wa fainali yao ya kutafuta bingwa wa Zanzibar wa mchezo wa Karata Zanzibar.

Maguji wa mchezo wa Karata kutoka Pemba na Unguja wakioneshana ufundi wa mchezo huo wa wahedi wasitini uliozikutanisha timu za Kibanda Mawazo ya Wawi Chakechake iliibuka Bingwa wa Mchezo huo kwa kuifunga Kilimahewa Star. kwa mizinga 4-2.

Baadhi ya wapenzi wa michezo ya Bao na Karata wakifuatilia fainali hizo za kutafuta Bingwa wa Zanzibar kwa michezo ya Asili Zanzibar hususan kwa Bao na Karata hupendwa sana Zanzibar.

Wapenzi wa mchezo wa Bao na Karata wakifuatilia michuano hiyo ya fainali katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Sharifa Khamis akizungumzia michuano hiyo ya fainali ya michezo Bao na Karata iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar. mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa Mchezo wa Karata na Bao Zanzibar akisoma risala ya michuano hiyo wakati wa fainali zake zilizofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar kwa kuzikutanisha timu kytoka Unguja na Pemba katika michuano ya fainali na kuto shukrani kwa mashirika yaliofanikisha michuano hiyo tangu mwazo hadi mwisho wa michuano hiyo na kupatika Bingwa wa michezo hiyo Zanzibar katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bihindi Hamad akizungumza wakati wa michezo ya fainali ya Bao na Karata katika viwanja vya Ekrotanali na kumkaribisha mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

Viongozi wa Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk Shein, akizungumza na wanamichezo ya Asili Zanzibar wakati wa fainali ya michezo hiyo iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali maisara Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wanamichezo wa michezo ya Bao na Karata Zanzibar wakati michuano wa michezo ya fainali iliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali Zanzibar na kupatikana mabingwa ni michezo hiyo. 

Washiriki wa michuano ya mchezo wakarata wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

Mshiriki wa mchezo wa Fainali ya michuano ya Bao na Karata akitowa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Bao Zanzibar Ndg Kidodi Salum Kidodi kwa kumshinda mpizani wake kutoka Jangombe Ndg Omar Othman kwa Bao 2-1, katika mchezo wa fainali uliofanyika katika viwanja vya Ekrotanali na kukabidhiwa Kombe na Fedha taslim shilingi laki tano.

Bingwa wa Zanzibar wa Mchezo wa Bao Ndg Kidodi Salum Kidodi akifurahia ubingwa wake. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi mshindi wa Pili wa Mchezo wa Bao Ndg Omar Othman Kombe na fedha taslim shilingi laki Tatu.












Saturday, September 26, 2015

MUZDALIFA YAENDELEZA KUENEZA MSAADA PEMBA

Jumuiya ya Muzdalifa yasaidia wananchi wa Pemba na watoto mayatima


JUMUIYA ya Kiislam ya Muzdalifa Charitable  Association Ofisi ya Pemba imechimba ng’ombe mia moja na ishirini (120)  na kuwapa sadaka wananchi wa Kisiwa cha Pemba wakiwemo watoto yatima .
Uchinjwaji wa ng’ombe hao umeenda sambamba na kusherekea sikuu ya Idd El Hajj inayosherekewa na waumini wa dini hiyo baada ya kukamilika kwa Ibada ya Hijja huko Macca.
Akizungumza  na mwandishi wa habari Mratibu wa Jumuiya hiyo Pemba Omar Hassan  amesema kuwa Jumuiya  yake imepokea msaada wa ng’ombe hao kutoka Jumuiya marafiki zilizoko Nchini Uturuki .
Amefahamisha kwamba kila mwananchi atafaidika na msaada wa nyama mijini na vijiji ambapo Jumuiya huwafikishia wananchi popote walipo bila a kujali imani ya dini , vyama wala kabila .
“Hii ni sadaka na inatakiwa kuwafikia waislamu wote , sisi Jumuiya tumepokea kutoka Jumuiya mbili  marafiki zilizoko Nchini Uturuki  , tunatoa bila ubaguzi pia tumewalenga zaidi watoto yatima ”alifahamisha .
Omar amewataka wananchi kutambua kwamba sadaka hiyo imetolewa kwa ajili yao , hivyo wanatakiwa kushirikiana na Jumuiya katika kufanikisha ugawaji wa sadaka na wale ambao hawatabahatika kupata waelewe kwamba haikuwa ridhiki yao .
“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Jumuiya , na tunatambua kutokana na jiografia ya Kisiwa cha Pemba baadhi ya maeneo hawatayafikia , hivyo wale ambao hawatabahatika waelewa haikuwa bahati yao ”alieleza .
Nao baadhi ya wananchi waliokutwa na mwandishi wa habari hizi katika eneo la machinjio ya Wete , wameishukuru Jumuiya hiyo kutokana na msaada huo na kusema  kuwa umekuja wakati muafaka .
Ali Khatib Chwaya akiwa katika chinjio hilo amesema kuwa Jumuiya hiyo imesaidia kukabiliana na changamoto ya kitoweyo kwa waumini wa Dini hiyo hasa katika kipindi hichi cha kusherekea Sikuu ya Idd El Hajj.
“Msaada huu umesaidia sana katika suala la kitoweyo hasa kwa watoto yatima na waislamu wengine wanaoishi kwenye mazingira magumu kwani umekuja wakati muafaka ”alisema Chwaya .
Aidha ameeleza kwamba wapo baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakirudi na kurudia kuchukua kitoweyo jambo ambalo linawafanya baadhi yao kukosa kupata sadaka hiyo ambayo imetolewa kwa wananchi wote .
Mchinjaji maarufu katika Mji Wete Shehe Haji amesema kuwa katika kusherekea Sikuu hiyo ya Idd El Hajj wamechimba ng’ombe sitini kwa siku ya kwanza na siku ya pili wakachinja ng’ombe sitini .
Kwa upande wake mkaguzi wa nyama kutoka Idara ya Mifugo Rashid Hamad ameeleza kwamba ng’ombe wote waliochinjwa walikuwa na afya njema na walikuwa wanafaa kwa matumizi ya binadamu .

Aidha mkaguzi huyo wa nyama  amewatoa hofu wananchi juu ya usalama wao kwa kusema kwamba ng’ombe wote waliochinjwa hawana madhara kwa watumiaji.
NA MOHAMED HEMED.

Idd el Hajj ilivyosherehekewa Tibirinzi Chake Chake Pemba

 WATOTO wakisherekea skukuu ya Eid El Hajj, kwa kupanda mja ya Pemba ya Ndege iliyomo ndani ya kiwanja cha kiwa katika maoja ya Pemba ya Ndege zilizomo ndani ya kiwanja cha Kufurahishia watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba.(Picha na Mohamed Hemed, PEMBA.)
 WATOTO wakionekana kufurahia pembea ya Farasi waliyokuwa wamepanda, wakati wa kusheherekea skukuu ya Eid El Hajj, huko katika kiwanja cha Tibirinzi Chake Chake Pemba.(Picha na Mohamed Hemed, PEMBA.)

  WATOTO wakisheherekea skukuu yao ya Eid EL Hajj, kwa kuendesha vigari vilivyomo ndani ya kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Mohamed Hemed, PEMBA.)
 WATOTO mbali mbali wakiwa kwenye foleni ya kusubiri kupanda pembea ya Wanda, ikiwa ni moja ya viburudisho vya watoto vilivyomo ndani ya kiwanja cha Kufurahishia watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba, katika skukuu ya Eid El Hajj.(Picha na Mohamed Hemed, PEMBA.)

 BAADHI ya ndugu na jamaa wakiwaangalia watoto wao wakipeperuka na pembea ya vikapu, wakati wa kusherekea skukuu ya Eid El Hajj katika kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba.(Picha na Mohamed Hemed, PEMBA.)

 WANAKIKUNDI cha maigizo kutoka Wete wakionesha umahiri wao wa michezo mbali mbali ya kuigiza, ndani ya eneo maalumu huko katika kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi chake chake Pemba, katika skukuu ya kwanza ya Eid El Hajj.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZAZI wakiwa katika foleni ya kuwakatia watoto wao tiketi za kupandia pembea mbali mbali, katika kiwanja cha kufurahishia wa watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba jana katika skukuu ya kwanza ya Eid El Hajj.(Picha na Mohamed Hemed, PEMBA.).
WANANCHI mbali mbali wakiwa katika foleni ya kuingia ndani ya kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba, wakati wa kusheherekea skukuu ya Eid El Hajj.(Pica na
Mohamed Hemed:)
bizoman.blogspot.com

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein Atowa Mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee wa Welezo na Sebleni Zanzibar

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar Bi Asha Abdalla wakiongozana na mlezi wa Wazee Welezo wakiwasili katika viwanja vya Makaazi ya Wazee Welezo Unguja kumuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kutowa Mkono wa Eid kwa Wazee hao kusherehekea Sikukuu hiyo ya Eid El Hajj.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha akizungumza na Wazee wa Welezo wakati alipofika katika makaazi yao kuwajulia hali na kutoa mono wa Eid El Hajj kwa Wazee hao kwa Niaba na Mama Mwanamwema Shein.
Wazee wa Makaazi ya Wazee Welezo Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha wakati alipofika katika makaazi ya Wazee Welezo kuwatembelea na kutoa Mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee hao.  
Wazee wa Makaazi ya Wazee Welezo Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha wakati alipofika katika makaazi ya Wazee Welezo kuwatembelea na kutoa Mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee hao
Kwa Niaba ya Wazee wanaoishi Makaazi ya Wazee Welezo Mzee Shein Kombo akitowa shukrani kwa niaba ya wazee wezake kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kwa kuwajali na kuwatembelea mara kwa mara anapopata nafasi kuja kuwajuliana hali na kujua shida zao,  
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee wa Welezo kwa Niaba ya Mama Mwanamwema Shein, 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akimjulia hali na kumpa mkono wa Eid El Hajj Mzee Chui anayeishi katika makaazi ya Wazee Welezo Zanzibar 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akimjulia hali Bi Riziki anayeishi katika Nyumba za Makaazi ya Wazee Welezo wakati alipowatembelea na kutoa mkono wa Eid kwa wazee hao kwa niaba na Mama Mwanamwema Shein.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif akizungumza na Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar, alipofika kuwatembelea na kutoa mkono wa Eid El Hajj kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein.  
Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha Balozi wakati alipowatembelea na kutoa mkono wa Eid El Hajj. 
Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha Balozi wakati alipowatembelea na kutoa mkono wa Eid El Hajj. 
Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha Balozi wakati alipowatembelea na kutoa mkono wa Eid El Hajj. 
Mzee Omar akisoma Dua wakati wa hafla hiyo 
Wazee wakiitikia dua. 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi akitowa mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee wa Nyumba Sebleni Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii Ndg Asha Abdalla akitowa mkono wa Eid kwa Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar kwa niaba ya Mama Mwanamwema Shein.
Imetayarishwa na: Mohamed Hemed: bizoman.blogspot.com

Thursday, September 24, 2015

Serikali kukabiiana na vitendo vyote vitakavyoashiria uvunjifu wa amani

 
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                 24.9.2015

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikaili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitaendelea kukabiliana na wale wote watakaofanya vitendo vitakavyoashiria kutaka kuvunja amani ya nchi wakati wote hasa katika kipindi hiki cha Kampeni za Uchaguzi Mkuu,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake ya Baraza la Idd al Hajj aliyoitoa huko katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alhaj Dk. Shein aliwahakikishia wananchi kuwa hakuna atakayeonewa au kudhulumiwa kwa njia yoyote ile lakini ni vizuri wajue kuwa Serikali ina wajibu wa Kikatiba wa kuwalinda watu wote na mali zao pamoja na wageni wanaoitembea Zanzibar.
Aidha, Alhaj Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa kisiasa, kijamii na wa madhehebu ya dini kuwasisitiza wafuasi wao umuhimu wa kuilinda amani na kujiepusha na vitendo vyote vitakavyoweza kuondoa amani na utulivu uliopo.
“Nimekuwa nikisema mara kadhaa kuwa amani haina mbadala. Bila ya amani hatuwezi kupata maendeleo yoyote”,alisisitiza Alhaj Dk. Shein.

Alhaj Dk. Shein alisema kuwa kutokuwepo kwa amani kunahatarisha uhai wa watu na ni sababu ya kuharibu miundombinu ya aina mbali mbali na kuzua fadhaa kwa jamii.
Aliendelea kueleza kuwa kutokuwepo kwa amani huwaondolea wasaa hata waumini katika kutekeleza ibada za kumuabudu Mola wao.
Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alisema kuwa Serikali imeanza kazi ya kufanya upembuzi yakinifu ili kuanzisha Mfuko wa Hijja Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia wananchi wengi zaidi waweze kupata fursa ya kuitekeleza ibada ya Hijja kwa wepesi na mapema zaidi.
Alisema kuwa Mfuko utakapoanzishwa watu wengi zaidi watapata nafasi na uwezo wa kuweka fedha kidogo kidogo kwa mujibu wa uwezo wao na hatimae watamudu kutekeleza ibada za Hijja na Umra kwa mujibu wa makubaliano na taratibu zitakazowekwa na Mfuko.
Aidha, Alhaj Dk. Shein alieleza kufarajika kwake na hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja katika sekta za kiuchumi, huduma za jamii na muamko wa wananchi katika kuzitumia fursa mbali mbali za kujiendeleza kiuchumi kwa kushirikiana na serikali.
Alhaj Dk. Shein alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa Mikoa inazidi kuimarika kiuchumi, kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na kuimarisha upatikanaji mzuri wa huduma za jamii, Serikali imeazimia kujenga mji wa kisasa katika Mkoa huo kwenye vijiji vya Matemwe na Kijini.
Pia, alisema kuwa ujenzi wa barabara wenye urefu wa kilomita 20.2 kutoka Matemwe kupitia Kijini hadi Kidoti umekwishaanza.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alisema kuwa wananchi wengi wa maeneo ya Bumbwini, Mkokotoni, Bwekunduni, Fungurefu na vijiji vyengine vya Mkoa huo wameimarisha uchumi wao kwa kujishughulisha na biashara ya madagaa ambayo husafirisha hadi Kongo na nchin nyengine  Jirani.
Akieleza mafanikio yaliofikiwa katika kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Mkoa huo Alhad Dk. Shein alisema kuwa upatikanaji wa  huduma hiyo imefikia asilimia 71.68.
Alisema kuwa mafanikio hayo yamefikiwa baada ya kutekeleza miradi mikuu mitatu ya maji safi na salama katika Mkoa huo ukiwemo Mradi wa Serikali kupitai Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mradi wa Ras-al-Khaiman na ADB.
Kadhalika Alhaj Dk. Shein alisema kuwa Serikali imeimarisha huduma za hospitali ya Koteji ya Kivunge pamoja vituo vya afya vyengine katika Mkoa huo ili kuziimarisha afya za wananchi.
Alhaj Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuzitaka taasisi zinazoshughulikia usafi wa miji ziongeze kasi katika kusafisha misingi ya maji machafu na njia za maji na usafi wa mazingira  ili kuepukana na mardhi katika kukabiliana na mvua za vuli zijazo ambapo kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa upo uwezekano wa kuwepo mvua kubwa za ‘El-Nino’.
Pia, Dk. Shein aliwanasihi wananchi kuacha kujenga katika sehemu za mabonde na wote wawe na moyo wa kusaidiana wakati wote, hsa pale Mwenyezei Mungu anapoleta mitihani mabali mbali.
Aidha, Alhaj Dk. Shein aliutaka uongozi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na taasisi zinazowasimamia madereva wachukue hatua madhubuti katika kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani katika Mkoa huo.
Mapema Alhaj Dk. Shein aliungana na wananchi katika Sala ya Idd-El-Hajj huko Katika uwanja vya Mpira Mkokotoni ambapo viongozi mbali mbali walihudhuria katika ibada hiyo pamoja na Baraza la Idd akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu Pili Balozi Seif Idd na viongozi wa dini, siasa, Serikali pamoja na wananchi.

Innaa Lillaahi Wainnaa ilayhi Raaji'uun : Zaidi ya Mahujaaj 200 wafariki leo wakati wakijiandaa kurusha vijiwe


Kiasi cha Mahujaaj wanaozidi 200 wamefariki asubuhi ya leo wakati walipokuwa wakielekea kwenye sehemu ya kurusha Vijiwe eneo la Mina nje kidogo ya Mji wa Makkah.

Mahujaaj wengine zaidi ya 400 pia walijeruhiwa wakati lilipotokea tukio hilo la mkanyagano wakati walipokuwa wakiingia katika moja ya (Tunnel) walipokuwa wakitoka Mina kuelekea eneo la Jamaraat ( kurusha vijiwe).  

Eneo la kurusha vijiwe bado ni eneo la hatari sana kutokea mkanyagano licha ya kutanuliwa na kuwekewa utaratibu mzuri wa kurusha vijiwe na Serikali ya Saudia.

Mpaka tunapoituma taarifa hii hatujapata taarifa zozote kwamba katika miongoni mwa waliotangulia mbele ya haki kuwamo Mahujaaj kutoka nyumbani.

Mola awasamehe madhambi yao, awarehemu kwa rehma yake na awaingize katika Jannatul Firdaus. Aamiyn

Baraza la Eid el Hajj Mkokotoni leo

Baraza la Eid el Hajj Mkokotoni leo

 Msafara wa Gari za  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein zikiongozwa na mapikipiki wakati ukiwasili katika Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskzani A Mkoa wa kaskazini Unguja palipofanyika mkutano wa baraza la Eid EL Hajj leo,[Picha na Ikulu.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa katiba na Sheria Mhe,Abubar Khamis Bakary mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo kabla ya kukagua gwaride rasmi la Sherehe hizo,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya Gwaride la KIKOSI cha Polisi FFU mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo (kushoto)Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame,[Picha na Ikulu.] 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi katika ukumbi wa  Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo,[Picha na Ikulu.] 

 Mke wa Makamo wa Pili wa rais wa zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (mwenye miwani) pamoja na Viongozi wengine mbali mbali wakiwa katika ukumbi wa  Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo,mgeni rasmi katika baraza hilo akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.] 
 Baadhi ya Viongozi na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.] 
 Baadhi ya Viongozi na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.]  
 Baadhi ya Viongozi wengine na Wazee na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Zanzibar katika Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini  Unguja ikiwa ni katika sherehe za Sikukuu ya Eid El Hajj,[Picha na Ikulu.]