Thursday, May 19, 2016

Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Makumbusho Duniani May18.

bizoman tayi

Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid  Ali Juma akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya kudumu ya sanaa katika  maadhimisho ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya  Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdalla akimuonyesha Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo sanaa ya ufumaji kofia za asili ya Zanzibar katika maonyesho ya sanaa yanayofanyika makumbusho ya Mnazimmoja.
Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akiangalia kazi ya ubunifu iliyofanywa na msanii Naaman Ali Khamis wa kwanza (kulia) anaetumia majani makavu ya migomba. 

Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho kutoka Idara ya Mkumbusho na Mambo ya Kale Khamis Abdalla akisoma risala ya wafanyakazi wa Idara hiyo katika ufunguzi wa maonyesho ya sanaa  ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Makumbisho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazimmoja Zanzibar.
Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rshid Ali Juma akizungumza na wafanyakazi na wananchi walioshiriki maonyesho ya sanaa katika maadhimisho ya ya siku ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazimmoja Zanzibar.

Baadhi ya viongozi wa Wizara na wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi wa maonyesho ya sanaa katika maadhimisho ya siku ya Makumbusho  Duniani yaliyofanyika  Mnazimmoja Mjini Zanzibar wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
(Picha na Makame Mshenga/Maelezo)

Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Habari, Utalili, Utamaduni na Michezo Zanzibar Rashid Ali Juma amewataka  wananchi wa Zanzibar kutumia fursa ya  kutembelea Jengo la Makumbusho  ya Mnazimmoja ili kuelewa historia ya  utamaduni  wao .

Waziri Rashid ameyasema hayo katika Sherehe za ufunguzi wa maonesho ya kudumu ya sanaa katika maadhimisho ya  siku ya makumbusho dunuani yaliyofanyika  Makumbusho ya Mnazi mmoja  Mjini Zanzibar.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  itaendelea kutoa misaada katika Idara ya Mkumbusho na Mambo ya kale ili isibakie nyuma katika ulimwengu  wa sasa  ambapo dunia imekuwa kama kijiji.

Waziri  wa Habari, Utalii Utamaduni na Michezo  amesema wananchi wanahitaji kutunza kumbukumbu na niwajibu kuyatunza maeneo  hayo yasipoteze haiba yake ya asili.

Katibu Mkuu  wa Wizara ya Habari, Utalili, Utamaduni na Michezo Zanzibar Omar Hassan Omar  amesema jengo la makumbusho ni muhimu na linapaswa kutuzwa  kwani mila, desturi na silka za Zanzibar  zinapotea  kutokana na  kukosekana  uhifadhi mzuri.

Aidha ameahidi  kushirikiana na wafanyakazi  wa Idara  hiyo kwa  kuwapatia mafunzo  ya mara kwa mara ili wawe na uwezo wa kutekeleza kazi  zao  kwa ufanisi zaidi .

Katika Risala yao iliyosomwa na Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Khamis Abdallah,  wafanyakazi hao wamesema  wameamua kuandaa maonyesho hayo ya kudumu ya sanaa ili kutoa mwamko na hamasa kwa jamii juu ya upana wa sanaa hiyo.

Wamesema wanajukumu kubwa la kulinda, kuhifadhi  na kutunza  kumbukumbu za taifa  lakini wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la maeneo ya kihistoria kuvamiwa na  wananchi.

“Tunajikuta tunajukumu kubwa kwa Serikali na hata kwa mwenyenzi mungu kuona kuwa rasilimali hizi zanaanza kupotea zikiwa  mikononi mwetu”,alisema Khamiss Abdallah.

Maonyesho hayo yamejumuisha  nyanja zote za maisha ikiwemo  Mavazi, Ususi, Ufinyanzi, Uhunzi, Uchoraji na Ujenzi  ikiwa ni utaratibu mzima wa mfumo wa maisha ya Wazanzibari.

Katuni na Ujumbe wake huuuooo....

Wednesday, May 18, 2016

Waziri wa Fedha Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed,Akisoma Hutuba ya ,Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

bizoman tayi

 

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa ajili ya kusoma Hutuba ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed akionesha Mkoba Wenye Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kusoma Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2016/2017. kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiingia katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi akiongozwa na Askari wa Baraza.kwa ajili ya kuaza kwa Mkutano wa Bajeti. 
Spika akingia katika ukumbi wa Mkutano jioni leo kwa ajili ya kuwasilishwa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. na Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed akiongozwa na Askari wa Baraza kuingia katika Ukumbi wa Mkutano kuwasilisha Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa  katika Ukumbi wa Mkutano wakati ikiwasilishwa Bajeti ya Serikali na Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed. kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Raya Issa Mselem na msaidizi wake wakifuatilia hutuba ya Bajeti ikiwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mopango Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed.jioni leo. 
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Dk Khalid Salum Mohammed akiwasilisha Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.















Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wakiwasili Mjengo kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Wawakilishi kusikiliza Hutuba ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka 2016/2017


Jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
 Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Juma Ali Khatib akiwa na Kiongozi wa Chama cha AD TADEA Mhe Mchenga wakiwasili katika viwanja vya Baraza kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wawakilishi ulioaza leo kwa hutuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Baraza kwa kusomwa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Mhe Nadir Abdullatif akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwasili katika viwanja vya Baraza kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Baraza.