Waziri
wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akikata utepe
kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya kudumu ya sanaa katika maadhimisho
ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazimmoja Mjini
Zanzibar.
Mkuu
wa Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdalla akimuonyesha Waziri
wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo sanaa ya ufumaji kofia za asili
ya Zanzibar katika maonyesho ya sanaa yanayofanyika makumbusho ya
Mnazimmoja.
Waziri
wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akiangalia kazi
ya ubunifu iliyofanywa na msanii Naaman Ali Khamis wa kwanza (kulia)
anaetumia majani makavu ya migomba.
Mkuu
wa Divisheni ya Makumbusho kutoka Idara ya Mkumbusho na Mambo ya Kale
Khamis Abdalla akisoma risala ya wafanyakazi wa Idara hiyo katika
ufunguzi wa maonyesho ya sanaa ikiwa ni maadhimisho ya siku ya
Makumbisho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazimmoja Zanzibar.
Waziri
wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rshid Ali Juma akizungumza
na wafanyakazi na wananchi walioshiriki maonyesho ya sanaa katika
maadhimisho ya ya siku ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya
Mnazimmoja Zanzibar.
Baadhi
ya viongozi wa Wizara na wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi wa
maonyesho ya sanaa katika maadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani
yaliyofanyika Mnazimmoja Mjini Zanzibar wakifuatilia hotuba ya mgeni
rasmi.
(Picha na Makame Mshenga/Maelezo)
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Habari,
Utalili, Utamaduni na Michezo Zanzibar Rashid Ali Juma amewataka
wananchi wa Zanzibar kutumia fursa ya kutembelea Jengo la Makumbusho
ya Mnazimmoja ili kuelewa historia ya utamaduni wao .
Waziri Rashid
ameyasema hayo katika Sherehe za ufunguzi wa maonesho ya kudumu ya sanaa
katika maadhimisho ya siku ya makumbusho dunuani yaliyofanyika
Makumbusho ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Amesema Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa misaada katika Idara ya
Mkumbusho na Mambo ya kale ili isibakie nyuma katika ulimwengu wa sasa
ambapo dunia imekuwa kama kijiji.
Waziri wa
Habari, Utalii Utamaduni na Michezo amesema wananchi wanahitaji kutunza
kumbukumbu na niwajibu kuyatunza maeneo hayo yasipoteze haiba yake ya
asili.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Utalili, Utamaduni na Michezo Zanzibar Omar Hassan
Omar amesema jengo la makumbusho ni muhimu na linapaswa kutuzwa kwani
mila, desturi na silka za Zanzibar zinapotea kutokana na kukosekana
uhifadhi mzuri.
Aidha ameahidi
kushirikiana na wafanyakazi wa Idara hiyo kwa kuwapatia mafunzo ya
mara kwa mara ili wawe na uwezo wa kutekeleza kazi zao kwa ufanisi
zaidi .
Katika Risala yao
iliyosomwa na Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Khamis Abdallah,
wafanyakazi hao wamesema wameamua kuandaa maonyesho hayo ya kudumu ya
sanaa ili kutoa mwamko na hamasa kwa jamii juu ya upana wa sanaa hiyo.
Wamesema
wanajukumu kubwa la kulinda, kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za taifa
lakini wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la maeneo ya kihistoria kuvamiwa
na wananchi.
“Tunajikuta
tunajukumu kubwa kwa Serikali na hata kwa mwenyenzi mungu kuona kuwa
rasilimali hizi zanaanza kupotea zikiwa mikononi mwetu”,alisema Khamiss
Abdallah.
Maonyesho hayo
yamejumuisha nyanja zote za maisha ikiwemo Mavazi, Ususi, Ufinyanzi,
Uhunzi, Uchoraji na Ujenzi ikiwa ni utaratibu mzima wa mfumo wa maisha
ya Wazanzibari.